1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz, Macron na Tusk kujadili sera za Ukraine

15 Machi 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anatarajiwa kukutana na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk, kujadili mengi juu ya sera ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4ddNj
Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Andreas Solaro/AFP/Getty Images

Scholz atakutana kwanza na Macron na baadae kufanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, na kisha viongozi hao wawili watakutana na Tusk.

Mazungumzo hayo yanafanyika karibu wiki tatu baada ya wakuu wa nchi takribani 20 kukusanyika mjini Paris kujadili mzozo wa Ukraine. Mkutano huo ulimalizika kwa tofauti ya mitizamo kuhusu uwezekano wa kupelekwa wanajeshi kwenye uwanja wa vita. 

EU yakubaliana kutoa euro bil. 5 kuinunulia silaha Ukraine

Mkutano huo ni wa kwanza wa ngazi ya juu kufanyika tangu Juni mwaka jana wa ushirika wa mataifa hayo matatu unaofahamika Weimar Triangle ambao uliundwa mwaka 1991.