1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Samuel Eto'o kugombea nafasi ya urais wa soka Cameroon

23 Septemba 2021

Mchezaji mashuhuri wa soka ulimwenguni, Samuel Eto'o anagombea nafasi ya urais katika shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon.

https://p.dw.com/p/40gpW
Samuel Eto'o Kamerun Nationalmannschaft Archiv 2013
Picha: Getty Images

Nyota huyo aliyewahi kuichezea timu ya Barcelona ameyaeleza hayo leo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Nafasi hiyo ilibaki wazi baada ya Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo kumuondoa katika nafasi hiyo rais wake Seidou Mbombo Njoya.

Eto'o alimuunga mkono Mbombo katika kampeni yake ya uchaguzi, lakini miaka miwili baada ya kustaafu kucheza mpira, nyota huyo mwenye umri wa miaka 40 alisema mapenzi yake kwenye mpira wa miguu yamemfanya kugombania katika kinyang'anyiro hicho.

Eto'o amesema itakuwa heshima kubwa kwake kuhudumu katika shirikisho hilo ambalo limesababisha apate sifa zote alizonazo hadi sasa.