1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RB Leipzig yatinga fainali ya DFB Pokal

Josephat Charo
3 Mei 2023

Klabu ya RB Leipzig imetinga fainali ya kombe la shirikisho la Ujerumani DFB Pokal kwa kuicharaza Freiburg 5-1 katika pambano kali la nusu fainali lilichezwa jana Jumanne mjini Freiburg.

https://p.dw.com/p/4Qp5y
SC Freiburg - RB Leipzig
Picha: Kai Pfaffenbach/REUTERS

Klabu ya RB Leipzig imetinga fainali ya kombe la shirikisho la Ujerumani DFB Pokal kwa kuicharaza Freiburg 5-1 katika pambano kali la nusu fainali lilichezwa jana Jumanne mjini Freiburg.

Kiungo mshambuliaji wa RB Leipzig Dani Olmo alitia kimyani bao la kwanza na kusaidia mabao mengine matatu kutiwa kambani wakati mabingwa hao watetezi wa kombe la shirikisho walipofuzu kwa fainali ya nne katika kipindi cha miaka mitano.

Leipzig inasubiri mechi ya leo ya nusu fainali ya pili kati ya Stuttgart na Frankfurt kujua itakwaana na nani katika fainali Juni 3.