1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UtamaduniTanzania

Rais Samia ahitimisha tamasha la Kizimkazi Zanzibar

1 Septemba 2023

Tamasha la Kizimkazi limefikia kilele chake leo huku likionekana kubadilisha taswira ya kijiji hicho alichozaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

https://p.dw.com/p/4Volv
Tansania Sansibar Präsidentin Samia Suluhu Hassan bei Kizimkazi Festival
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiteza jambo na Waziri Mkuu Kaasim MajaliwaPicha: Presidential Press Service Tanzania

Mabadiliko hayo yakifuata mtazamo wa kijiji cha Chato Tanzania Bara kilichopata mabadiliko makubwa na ya haraka muda mfupi akiwa madarakani aliekuwa rais wa awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli. 

Rais Samia amerithi kama ilivyokuwa kwa Rais Magufuli alipokuwa madarakani nguvu kubwa zilielekezwa kwenye kijiji chake alichotoka huku taasisi za kifedha, makampuni na wawekezaji kuwekeza fedha zao kwenye miradi mbali mbali kijijini hapo.
Akizungumza katika ufungaji wa tamasha hilo Rais Samia alisema amevutiwa na washirika wa maendeleo na mashirika mbalimbali ya kifedha kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua sekta za elimu, afya, uvuvi, utalii, utamaduni na michezo

Soma zaidi:Rais wa Zanzibar ateuwa Tume ya Uchaguzi

Aidha amesisitiza kuwalinda watoto kimaadili kama kauli mbiu inavyosema ‘tuwalinde kimaadili watoto wetu kwa maslahi ya taifa’ 

Kijiji cha Kizimkazi chenye wakaazi takriban 7,000 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 kilichosheheni vivutio vya utalii ikiwemo hifadhi ya msitu wa jozani, fukwe, mapango ya asili, msikiti mkongwe, na kuongezewa na wanyama kutoka upande wa Tanzania bara kama Simba.

Maeneo ya utalii yazinduliwa

Kizimkazi ipo katika mkoa wa kusini Unguja na mwaka huu pekee kimepata miradi mingi mikubwa zaidi ya kumi ikiwemo ujenzi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano.

kando na hayo upatikanaji wa maji safi umeimarishwa, ujenzi wa shule na zahanati kadhaa pamoja na uwanja wa kufurahishia watoto ambao unakadiriwa kutumia mabilioni ya fedha.

Tansania Sansibar Präsidentin Samia Suluhu Hassan bei Kizimkazi Festival
Rais wa Tanzania Samia Suluhu akiwa na viongozi wengine katika tamasha la kizimkazi Picha: Presidential Press Service Tanzania

Naye Katibu wa Kamati ya Tamasha la Kizimkazi, Hamid Abdulhamid amesema miradhi kadhaa zaidi ilifunguliwa ili kuimarishwa ustawi wa kijiji hicho.

Hili ni tamasha la nane lakini ni la pili kwa ukubwa tokea Rais Samia kuingia madarakani ambalo limebeba ujumbe wa Tamasha la Kizimkazi lilianzishwa mwaka 2015 likianzia na siku ya Samiana baadae kuongezewa ukubwa miradi na sherehe tofauti pamoja na kushirikisha utamaduni wa asili ikiwemo vyakula, ngoma, muziki wa taarab na kizazi kipya.

Soma zaidi:Wadau wahimizwa kukitumia Kiswahili katika tafiti

Burudani zingine ambazo zilitawala tamasha hilo ni pamoja na mpira wa miguu, resi za ngarawa na mchezo wa ngumi ambao kwa mara ya kwanza umefufuliwa baada ya kupigwa marufuku zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Tamasha hilo limehudhuriwa na viongozi wakuuwa Tanzania na Zanzibar akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaaliwa, Makamo wa kwanza wa Rais Othman Masoud na Spika wa Bunge na wa baraza la wawakilishi.