1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

QUAD lina hofu ya shughuli za kijeshi katika bahari ya China

Iddi Ssessanga
3 Machi 2023

Marekani, Japan, India na Australia zimetaja leo wasiwasi wao juu ya shughuli za kijeshi katika bahari ya China baada ya kuzuka kwa mvutano kati ya Washington na Beijing.

https://p.dw.com/p/4OCXy

China imekuwa ikidai kuwa na mamlaka kamili juu ya eneo kubwa la bahari hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa mengine matatu kutoka kundi la QUAD walikutana kwa mazungumzo mjini New Delhi.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na mwenyeji wa mkutano huo India, Quad imesisitiza kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria za kimataifa katika Bahari ya Mashariki na Kusini mwa China ili kukabiliana na changamoto kwa utaratibu wa misingi ya sheria za baharini.