1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pande hasimu Libya zashindwa kuafikiana kuhusu uchaguzi

1 Julai 2022

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya Stephanie Williams amesema maafisa wawili waandamizi kutoka kambi zinazohasimiana nchini Libya wameshindwa kufikia makubaliano ya kikatiba kwa ajili ya uchaguzi nchini humo.

https://p.dw.com/p/4DXY0
Schweiz Libysches Dialogforum in Genf
Picha: UNITED NATIONS/AFP

Williams amesema spika mwenye ushawishi wa bunge lililo mashariki mwa nchi hiyo Aguila Saleh, na Khaled al-Meshri ambaye ni mkuu wa Baraza Kuu la serikali iliyoko magharibi, hawakukubaliana kuhusiana na vigezo vya wagombea urais katika mazungumzo ya siku mbili mjini Geneva.

Mazungumzo hayo ya Geneva ndiyo juhudi za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa kuziba mapengo yaliyopo kati ya pande hizo mbili baada ya mazungumzo ya awamu ya kwanza mjini Cairo kugonga mwamba.