1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Biashara

Makampuni ya Ujerumani yakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi

Bruce Amani
29 Novemba 2023

Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda nchini Ujerumani - DHIK kimesema nusu ya makampuni ya Ujerumani yanakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi, licha ya kudorora kwa taifa hilo kubwa kiuchumi katika kanda ya sarafu ya euro.

https://p.dw.com/p/4ZZPk
Kiwanda cha kuunda magari cha Audi
DHIK inasema nusu ya kampuni za Ujerumani zinakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi.Picha: Hugo Ortuno/EPA/picture alliance

Ujerumani, kama tu ilivyo katika nchi nyingine zilizostawi kiviwanda kote duniani, inakabiliwa na uhaba mkubwa wa wafanyakazi, hasa katika sekta za ujuzi wa ukuaji wa juu.

Soma pia: Ujerumani kuwa nchi ya pekee barani Ulaya kuingia kwenye mdororo wa uchumi 2023

Achim Dercks, Naibu Afisa Mkuu Mtendaji wa DHIK amesema hali ya upatikanaji wa wafanyakazi wenye ujuzi bado ni mbaya sana. Kwa mujibu wa makadirio ya karibuni, nafasi za ajira milioni 1.8 hazijajazwa katika uchumi wa Ujerumani kwa ujumla.

Dercks anasema hiyo inamaanisha zaidi ya euro bilioni 90 katika thamani ya ziada zitapotea mwaka huu. Hii ni sawa na zaidi ya asilimia mbili ya pato jumla la nchi.