1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yalenga kubeba taji la AFCON

5 Februari 2024

Mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen amesema kwamba timu yake inalenga kuendeleza rekodi yake kwenye michuano hii ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakapomenyana na Afrika Kusini katika nusu-fainali.

https://p.dw.com/p/4c4VH
AFCON
Mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen (Kulia) akisherehekea ushindi dhidi ya Angola. Picha: Issouf Sanogo/AFP

Wenyeji Ivory Coast wakikutana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Tangu sare ya 1-1 na Equatorial Guinea katika mechi yao ya ufunguzi, Nigeria wameandikisha ushindi mara nne mfululizo bila kuruhusu bao. Nigeria imefuzu kwa nusu fainali ya 15 ya Kombe la Mataifa Afrika huku wakilenga kunyanyua kombe hilo kwa mara ya nne tangu 2013 nchini Afrika Kusini.

Soma pia: Mechi za nusu fainali za AFCON kutifua vumbia kuanzia Jumatano

Afrika Kusini walijikatia tiketi ya nusu finali baada ya mlinda lango Ronwen Williams kupangua mikwaju minne ya penalti kutoka kwa Cpe Verde siku ya Jumamosi. Bafana Bafana hawakufuzu kwa AFCON ya mwaka 2022, lakini wamerejea kwenye hatua kubwa chini ya kocha mkongwe wa Ubelgiji Hugo Broos.Broos aliiongoza Cameroon kunyakua taji la 2017 na sasa ameifikisha Afrika Kusini katika nusu fainali ya kwanza baada ya miaka 24.

Wenyeji Ivory Coast watamenyana na DR Congokatika nusu fainali ya pili kwenye Uwanja wa Olympic wa Ebimpe mjini Abidjan, ambapo Ivory Coast ilichezea kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Guinea ya Ikweta katika mechi yao ya mwisho ya makundi.

Ivory Coast itawakosa Odilon Kossounou na Oumar Diakite, lakini Sebastien Haller anatarajiwa kuanza kwa mara ya kwanza kwenye michuano hii. DR Congo iliishinda Misri kwa mikwaju ya penalti katika hatua ya 16 bora na ikatoka nyuma na kuifunga Guinea 3-1 katika robo fainali na wana ndoto ya kufika fainali kwa mara ya kwanza tangu walipotwaa ubingwa wakiwa Zaire mwaka 1974.