1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yakwaaa na Afrika Kusini nusu fainali AFCON

7 Februari 2024

Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yanaingia hatua ya nusu fainali huku mabingwa mara tatu Nigeria wakipambana na Afrika Kusini majira ya saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/4c8fu
Mashabiki wa soka kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayochezwa Ivory Coast.
Mashabiki wa soka kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayochezwa Ivory Coast.Picha: Marco Simoncelli/DW

Nigeria wamepewa nguvu na kurudi kikosini kwa mshambuliaji wao, Victor Osimhen, ambaye kwa siku kadhaa hakufanya mazoezi.

Wanapambana na Afrika Kusini yenye idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza katika ligi ya nyumbani na ambao waliiondoa Moroko kutoka kwenye mashindano hayo katika hatua ya robo fainali.

Baadaye leo, wenyeji Ivory Coast walioipeleka nyumbani Mali, watakuwa wanapambana na wawakilishi wa Afrika Mashariki - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - katika nusu fainali ya pili.

Kongo ilitingi nusu fainali baada ya kuibwaga Guinea.