1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria na DR Kongo zashinda na kufuzu nusu fainali AFCON

Iddi Ssessanga
3 Februari 2024

Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimefuzu nusu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, AFCON, kwa ushindi dhidi ya Angola na Guinea.

https://p.dw.com/p/4bzmU
Kombe la Mataifa ya Afrika 2024 I Nigeria vs Angola
Nigeria imefuzu Nusu Fainali ya AFCON kwa kuipiga Angola wahedi sifuri.Picha: Franck Fife/AFP

Nigeria imefuzu hatua hiyo kwa bao pekee lililofungwa na mshambuliaji wa klabu ya Atalanta, Ademola Lookman, dakika nne kabla ya kumazikiza kwa kipindi cha kwanza, katika uwanja wa Felix Hofet Boiny.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imetokea nyuma na kuishinda Guine kwa mabao 3-1 katika uwanja wa Ebimpe Olympic mjini Abidjan.

Nigeria sasa itasubiri kati ya Cape Verde na Afrika Kusini, kujua mpinzani wake wa nusu fainali Jumatano ijayo, huku DR Kongo ikisubiri kati ya Mali na wenyeji Ivory Coast.

Mechi mbili za kuamua washiriki wengine wa nusu fainali zinachezwa jioni ya leo.