1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu: Israel iko karibu kushinda vita dhidi ya Hamas

Amina Mjahid
7 Aprili 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema nchi yake inakaribia kushinda vita vyake dhidi ya wanamgambo wa Hamas katika ukanda wa Gaza

https://p.dw.com/p/4eWAf
 Israel Tel Aviv | Benjamin Netanjahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Ronen Zvulun/AFP/Getty Images

Netanyahu ameapa kuwa makubaliano haytokuwepo hadi kundi hilo litakapowaachia mateka wote inaowashikilia.  

Akizungumza na Baraza lake la mawaziri hii leo wakati vita hivyo vikiingia mwezi wake wa sita, Netanyahu amesema Israel haiwezi kuyakubali matakwa ya Hamas.  

"Kusalimu amri mbele ya Hamas yatalifanya kundi hilo kujaribu kurudia walichokifanya Oktoba 7 kama ilivyoahidi kufanya. Hamas inadhani kuwa shinikizo kutoka nje na ndani ya Israel kutafanya tuyakubali matakwa yao. hilo halitotokea. Badala ya shinikizo kuelekezwa Israel jumuiya ya kimataifa inapaswa kuelekeza shiniko hilo kwa Hamas. na hii itasaidia kuachiwa kwa mateka," alisema Benjamin Netanyahu.

Biden azirai Misri na Qatar zishinikize kuachiwa mateka

Hamas ilithibitisha kwamba moja ya matakwa yake katika mazungumzo hayo ni kusitishwa kabisa mapigano mjini Gaza na wanajeshi wa Israel kuondoka huko.

Mapigano kati ya Israel na Hamas yalianza Oktoba saba wakati wanamgambo hao walipovamia kusini mwa Israel na kusababisha mauaji ya waisraeli 1,200 nayo Israel ikaanzisha mashambulizi katika ukanda wa Gaza na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu 32,000