1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Navalny anaugua maradhi yasiyojulikana jela

13 Aprili 2023

Msemaji wa kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny, Kira Yarmysh, anasema mwanasiasa huyo anaugua maradhi yasiyojulikana, ambayo huenda ikawa yamesababishwa na kulishwa sumu inayofanya kazi taratibu.

https://p.dw.com/p/4PzSt
FIlmstill l Dokumentarfilm  Navalny
Picha: Warner Bros. Pictures via AP/picture alliance

Yarmysh anasema Navalny ambaye yuko gerezani amepunguza kilo nane katika kipindi cha zaidi ya wiki mbili tu. Msemaji huyo ameongeza kwamba Navalny amewekwa katika seli ambapo anapokea adhabu huku akiwa na maumivu makali bila kupata msaada wowote wa kimatibabu.

Mwaka 2020,  Navalny aliponea shambulizi la sumu wakati alipokuwa safarini kuelekea Siberia ambapo uchunguzi wa maabara ulionyesha kwamba alikuwa amelishwa sumu. Urusi inakanusha kwamba serikali ilijaribu kumuua.

Alitibiwa kwa sumu hiyo nchini Ujerumani ila akarudi Urusi kwa hiari na akatiwa nguvuni mara tu alipowasili na kufungwa jela kwa kesi ya ufisadi ambayo anasema ilichochewa kisiasa.