1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Naibu Waziri Mkuu wa Ethiopia afutwa kazi

26 Januari 2024

Naibu Waziri Mkuu wa muda mrefu wa Ethiopia, Demeke Mekonnen, ameachishwa kazi leo kama makamu wa rais wa chama tawala nchini humo, na kuzua mashaka juu ya jukumu lake la baadaye katika serikali.

https://p.dw.com/p/4bjR5
Ethiopia | Demeke Mekonnen Hassen
Demeke Mekonnen Hassen afutwa kazi umakamu mwenyekiti wa chama tawala Ethiopia.Picha: Graham Carlow/Creative Commons

Shirika la habari la serikali, FANA, limeripoti kuwa nafasi ya Demeke, ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje na anayetokea katika kabila ya Amhara, imechukuliwa na mkuu wa kijasusi wa Ethiopia.

Soma zaidi: Waziri mkuu wa Ethiopia aahidi mageuzi

Shirika hilo la habari limeongeza kuwa chama tawala "kimemchagua kwa sauti moja" Temesgen Tiruneh, ambaye anaongoza idara ya ujasusi na usalama, katika mabadiliko yanayotajwa kufuata "kanuni ya urithi wa uongozi na mfumo wa uendeshaji."

Hatua hiyo pia imeripotiwa na shirika rasmi la habari la Ethiopia, ENA.

Soma zaidi: Chama tawala Ethiopia chamchagua kiongozi mpya

Kubadilishwa kwa Demeke ndani ya chama kunamaanisha kuondoka kwake kama naibu waziri mkuu pia, chanzo cha karibu na Waziri Mkuu Abiy Ahmed kimeliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina.