1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muhoozi atangaza azma ya kuchukua urais wa Uganda

28 Oktoba 2022

Kwa mara nyingine mtoto wa kiume wa rais Yoweri Museveni wa Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba ameibua mjadala baada ya kutangaza kwamba anaazimia kuwa rais wa Uganda na atafanya hivyo kwa heshima ya mamake.

https://p.dw.com/p/4InW4
Uganda Kampala | Muhoozi Kainerugaba
Picha: Peter Busomoke/AFP/Getty Images

Kulingana na wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kisiasa, ujumbe huo unaiweka Uganda katika joto la kisiasa  ikiwa imesalia miaka mitatu na nusu kabla ya kuwadia msimu wa uchaguzi kuwadia.

Hapo awali, dalili za Jenerali Muhoozi kuonyesha nia yake kuwa rais wa Uganda hazikutiliwa maanani na wengi. Lakini kufuatia ujumbe wake kwenye jukwaa lake la Twitter siku ya Alhamisi ni dhahiri kwamba azma hiyo imekuwepo na anaizingatia kwa dhati. Katika ujumbe huo ametaja kuwa anataka kuwa rais wa Uganda na hilo litatokea.Museveni amuondoa mwanae ukuu wa jeshi, ampandisha cheo

Uganda Kampala | Auszeichnung Muhoozi Kainerugaba als Generalleutnant
Muhoozi wakati akipewa cheo cha Luteni Kanali mwaka 2019Picha: Joseph Kiggundu/Photoshot/picture alliance

Ameongezea kusema kuwa hii itakuwa ni kwa heshima ya mamake Janet Museveni ambaye katika ujumbe uliotangulia  huo alimtaja kuwa malaika wake asiye na mfano. Ujumbe huu umewatumbukiza raia mbalimbali katika mjadala kuhusu nini anachopanga Jenerali Yoweri Museveni kuhusiana na urithi kwa wadhifa wa  urais. Wambede Wamoto ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa ametoa mtazamo huu.

Hivi karibuni makundi mbalimbali ya vijana yameshuhudiwa yakifanya maandamano ya kumuunga Jenerali Muhoozi kuwania urais. Wao huvalia fulana na kuonyesha mabango yenye ujumbe huo wakipitia barabara za miji mbalimbali.  Ijapokuwa rais Museveni mwenyewe hajataja nia yake kuwania urais mwaka 2026, bado anayo fursa hiyo kufuatia hatua ya kuondolewa kwa ukomo wa umri kwa mgombea urais nchini Uganda. Haya ni baadhi ya maoni ya vijan.

Museveni akosolewa kuhusu kumteua mwanae

Hapo awali maafisa wa jeshi walioonyesha nia ya kushiriki siasa walichukuliwa hatua za kisheria na kufunguliwa mashtaka au kuwekwa katika vizuizi. Miongoni mwa ni Jenerali Henry Tumukunde na Sejusa. Lakini hakuna hatua za kisheria zimechukuliwa kwa jenerali Muhoozi ambaye angali afisa wa kijeshi na kwa mtazamo wa wachambuzi hii inaleta  mkanganyiko katika taasisi hiyo kuhusiana na uhusika wao katika siasa za nchi. Wamoto anaongezea hivi….

Licha ya rais Museveni kumtaka mwanawe asiendelee kutumia mitandao ya kijamii kusambaza ujumbe wenye hisia za kisiasa, ujumbe huo wa hapo jana unaonyesha kuwa Jenerali Muhoozi hajazingatia ushauri wa babake. Lubega Emmanuel DW Kampala.