1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya AFCON yaelekea ukingoni

Amina Mjahid
10 Februari 2024

Mechi ya kuwania nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika AFCON itatimua vumbi leo (10.02.2024) Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo itachuana na Afrika Kusini.

https://p.dw.com/p/4cFxF
AFCON | Abidjan
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo itachuana na Afrika Kusini kuwania nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika AFCON Picha: Braima Darame/DW

Kesho Jumapili (11.02.2024)katika uwanja wa Ebimpe mjini Abidjan wanakosubiriwa mashabiki karibu 60,000, kutashuhudiwa fainali kati ya Nigeria na wenyeji Ivory Coast.

Nigeria ilishindwa mara tano kati ya mara sita katika hatua ya nusu fainali za michuano hiyo huko nyuma na sasa itakabiliana na wenyeji Ivory Coast katika fainali hizo zitakazochezwa siku ya Jumapili.

Ivory Coast ambao ni mabingwa mara mbili wa AFCON ni wenyeji wa kwanza wa michuano hiyo kuingia fainali tangu Misri ilipoingia fainali za mwaka 2006, na hatua hii imewashangaza wengi kwa kuwa timu hiyo ilikuwa hatarini kutolewa katika hatua za makundi.