1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiColombia

Medellín Colombia: Ukahaba wapigwa marufuku kwa miezi sita

Tatu Karema
2 Aprili 2024

Meya wa jiji la Medellín nchini Colombia Federico Gutiérrez amepiga marufuku ukahaba katika baadhi ya vitongoji maarufu vya mji huo kwa miezi sita kuzuia unyanyasaji wa kingono kwa watoto

https://p.dw.com/p/4eK4m

Katika mkutano na wanahabari, Gutiérrez amesema marufuku hiyo itatekelezwa katika vitongoji vya Provenza na El Poblado, maeneo mawili ya mji huo yenye idadi kubwa ya mabaa na vilabu ambavyo pia ni maarufu kwa maelfu ya watalii.

Gutiérrez asema watoto wadogo hulazimishwa kufanya ukahaba

Maeneo hayo pia yana idadi kubwa ya makahaba wanaotafuta wateja wa kimataifa.

Gutiérrez amesema kuwa mitandao ya wahalifu huwapeleka watotowadogo katika maeneo hayo na kuwalazimisha kufanya ukahaba.

Meya huyo ameongeza kuwa ni lazima kulidhibiti eneo hilo na kuilinda jamii.