1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya kiarabu yafanya mkutano wa kujadili hali ya Gaza

11 Novemba 2023

Mataifa ya ya kiarabu yanatarajiwa kufanya mkutano wa dharura mjini Riyadh leo Jumamosi ulioitishwa kwa maombi kutoka Palestina na Saudi Arabia kujadili kile nchi hizo umekiita "uchokozi wa Israel dhidi ya Gaza".

https://p.dw.com/p/4Yh9E

Viongozi wa mataifa 22 yanayounda Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na wengine kutoka mataifa ya kiislamu akiwemo rais wa Iran,  Ebrahim Rais watashauriana, namna ya kukabiliana na mzozo unaoendelea katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa hayo waliokutana siku ya Alhamisi kwa maandalizi ya mkutano wa leo, walilaani hujuma za Israel kwenye ukanda wa Gaza na kutaka nchi hiyo iwajibishwe kwa uhalifu dhidi ya watu wa Palestina.

Vita vinavyoendelea Gaza vilianza baada ya kundi la Hamas kuwauwa raia 1,200 wa Israel katika shambulio la kushtukiza lililofanywa Oktoba 7.