1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani, Uingereza zataka uchaguzi huru Sudan Kusini

20 Machi 2024

Mataifa ya Marekani, Uingereza na Norway yameto mwito kwa viongozi wa Sudan Kusini kuchukua hatua za haraka, ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa amani unafanyika mnamo mwezi Disemba.

https://p.dw.com/p/4dv2N
Juba, Sudan Kusini | Rais Salva Kiir
Rais Salva Kiir wa Sudan KusiniPicha: Samir Bol/ZUMAPRESS/picture alliance

Hayo ni katika taarifa ya pamoja kufuatia onyo la Marekani kwamba taifa hilo la Afrika Mashariki haliko katika mwelekeo wa kufanya uchaguzi huru na wa haki, ispokuwa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti.

Mataifa hayo yamesema kuwa kutochukuliwa hatua madhubuti na kutokuruhusu kufanyika kwa uchaguzi huo muhimu ni kushindwa kwa viongozi wa taifa hilo ambalo lilishuhudia mzozo wa kiutawala.

Soma pia:Idadi ya walioathiriwa na ghasia yaongezeka kwa 35% Sudan Kusini

Sudan Kusini inapanga kuchagua viongozi watakaorithi serikali ya mpito ya sasa, inayoongozwa kwa pamoja na Rais Salva Kiir na Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar, ambao vikosi vyao vilipambana wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo 2013-2018.
 

Kwa habari nyingine zaidi za ulimwengu, karibu kwenye chaneli yetu ya YouTube.