1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Wito wa msaada watolewa Malawi kufuatia kimbunga Freddy

16 Machi 2023

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ameomba msaada wa kimataifa wa kukabiliana na "janga la kitaifa" baada ya Kimbunga Freddy kupiga taifa hilo na kusababisha vifo vya mamia ya watu na uharibifu mkubwa.

https://p.dw.com/p/4OkjY
Malawi Präsident Lazarus Chakwera
Picha: AMOS GUMULIRA/AFP

Wakati akitangaza maombolezo ya kitaifa ya wiki mbili, rais Chakwera amesema kiwango cha uharibifu wanachokabiliana nacho ni kikubwa mno kuliko rasilimali walizo nazo.

Waokoaji waendelea kupambana kuwafikia manusura wa kimbunga

Serikali ya Malawi imeahidi kutoa dola milioni 1 na nusu ili kuwasaidia maelfu ya waathiriwa wa kimbunga hicho ambacho kimesababisha nchini Malawi pekee vifo vya watu wapatao 225 na kuwajeruhi mamia ya wengine.

Kimbunga Freddy kimesababisha hadi sasa vifo vya karibu watu 290 katika nchi za Malawi na Msumbiji.