1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makomandoo wa Israel wawauwa Wapalestina hospitalini

30 Januari 2024

Makomandoo wa Israel waliojifanya Wapalestina wameivamia hospitali moja Ukingo wa Magharibi leo na kuwauwa wananaume watatu wa kipalestina wakimtuhumu mmoja kati yao kupanga shambulizi kubwa na wengine kushiriki ghasia.

https://p.dw.com/p/4bqDj
Ukanda wa Gaza | Wahudumu wa afya wakiwa katika majukumu yao
Wahudumu wa afya wakiwahudumia wagonjwa katika eneo la Ukanda wa Gaza.Picha: European Broadcasting Union

Mikanda ya video kutoka kamera za kufuatilia nyendo imewaonesha wanajeshi kadhaa wa Israel ikiwemo watatu waliovalia mavazi ya kike na wengine waliojifanya kuwa wauguzi wakikatisha ndani ya hospitali ya Ibn Sina iliyo kwenye mji wa Jenin wakiwa wamebeba bunduki za rashasha.

Maafisa wa polisi wa Israel wamesema watu hao watatu waliuwawa katika operesheni ya siri na mmoja ametajwa kuwa mwanamgambo wa kundi la Hamas aliyehusika na kupanga shambulizi mfano wa lile la Oktoba 7 dhidi ya Israel.

Soma pia:Wapalestina watatu wauwawa Ukingo wa Magharibi

Wizara ya Afya ya Palestina imesema wanajeshi waIsrael walifyetua risasi ndani ya wodi za hospitali na imetoa mwito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuizuia Israel kuendesha operesheni zake kwenye majengo ya hospitali.