1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yabatilisha maamuzi ya chadema kuhusu wabunge 19

14 Desemba 2023

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imewapa ushindi wabunge 19 wa viti maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) waliokuwa wakipinga uamuzi wa baraza kuu la chama hicho la kuwafuta uanachama.

https://p.dw.com/p/4aA9I
Siasa | Wabunge 19 wa Chama Kukuu cha Upinzani Tanzania Chadema.
Wanachama na wabunge wa Chadema waliofukuzwa uanachama wakitoka nje ya chumba cha mkutano wa Baraza Kuu la ChademaPicha: Eric Boniphace/DW

Akisoma Hukumu hiyo Jaji Cyprian Mkeha amesema kitendo cha wajumbe wa Kamati Kuu iliyowafukuza kuwa tena wajumbe wa Baraza kuu ambalo lilisikiliza rufaa yao kinaondoa uhalali wa maamuzi ya Baraza Kuu "Baraza Kuu lilikwenda kinyume na kanuni ya kawaida ya kutokupendelea

Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa hatimaye leo imewadia baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, kuridhia kuwa utaratibu wa kuwafukuza uanachama wabunge 19 wa viti maalum wa Chadema haukuwa sahihi kwa mujibu wa katiba hukumu inayowapa uhalali wa kuendelea kuwa wanachama na kubaki na ubunge wao.

Jaji katika kesi hiyo, Chrispian Mkeha amesema Halima Mdee na wenzake 18, wataendelea kuwa wanachama wa Chadema kwa kuwa Baraza Kuu la chama hicho lilikwenda kinyume na Kanuni ya Kawaida ya kutokupendelea.

 Soma pia:CHADEMA yawatimua wanasiasa 19 kwa makosa ya usaliti

Malalamiko ya Mdee na wenzake, ni kutaka baraza kuu la chadema liwape muda wa kuwasikiliza badala ya kuchukua maamuzi ya kuwavua uanachama pasi ya kuwapa haki ya kuwasikiliza.

Vuta n'kuvute hii ilianza mapema mwaka 2020 mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu ambapo chadema kilipata uwakilishi mdogo bungeni na kuambulia kiti kimoja cha ubunge na viti maalum 19.

Ushindi huo mwembamba uliifanya Chadema kususia matokeo hayo na kuweka msimamo mmoja wa kususia hata shughuli za bunge. Hata hivyo wabunge hawa 19, waliamua kuingia bungeni na kuendelea na shughuli za bunge, huku Chadema kikisema hakitambui uwakilishi huo.

Wabunge kumi na tisa kuvuliwa uanachama

Baadaye Novemba, 2020, kamati kuu ya  Chadema, liliamua kuwafuta uanachama wabunge hao, uamuzi ambao kimantiki, unawaondolea hadhi ya kuwa wabunge kikatiba.

Wabunge hao wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema BAWACHA Halima Mdee, walikata rufaa katika Baraza Kuu la Chadema  kupinga uamuzi wa kamati kuu kuwafukuza uanachama hata hivyo Baraza Kuu nalo lilitupilia mbali rufaa hiyo, na kupelekea wabunge hao  kukimbilia mahakamani.

Soma pia:Spika wa bunge Tanzania asema wabunge wa viti maalum ni halali

Hata hivyo, Wabunge hao 19 hawakuwepo mahakamani kwa madai kuwa wanawakilishwa na mawakili wao na mmoja wa walalamikaji hao.

Katika kesi hiyo, Mdee na wenzake, walitetewa na jopo la mawakili wakiongozwa na wakili Ipilinga Panya, huku Chadema kikiongozwa na Wakili Tito Magoti.

Shinikizo ndani ya Chama cha Chadema ili wabunge waso watiifu wafukuzwe