1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Mahakama Senegal yakataa maombi ya Sonko kuwania urais

6 Januari 2024

Baraza la Katiba nchini Senegal limetupilia mbali maombi ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwezi ujao ya kiongozi wa upinzani aliye gerezani Ousmane Sonko.

https://p.dw.com/p/4avKT
Mea wa jiji la Zinguinchor Ousmane Sonko akabiliwa na kesi kadhaa mahakamani zinazotishia ugombeaji wake kiti cha urais
Mea wa jiji la Zinguinchor Ousmane Sonko akabiliwa na kesi kadhaa mahakamani zinazotishia ugombeaji wake kiti cha urais Picha: Cooper Inveen/REUTERS

Mwanasheria wa Sonko, Cire Cledor Ly, amesema baraza hilo limearifu kwamba nyaraka hizo za Sonko hazikukamilika lakini hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu hoja hiyo.

Amesema jopo la mawakili wa mwanasiasa huyo huenda litawasilisha malalamiko ya kupinga uamuzi huo pindi watakapopatiwa maelezo ya kina.

Sonko mwenye umri wa miaka 49 amekuwa kwenye mvutano  na mamlaka za Senegal kwa zaidi ya miaka miwili kuhusiana na mipango yake ya kuwania urais wa mwaka huu.

Amekabiliwa na vizingiti vingi ikiwemo kesi iliyopelekea kufungwa jela mwezi Juni mwaka jana. Serikali ilitumia hukumu hiyo ya kifungo kumnyima fomu za kuwania urais lakini aliwasilisha maombi yake kwa Baraza la Katiba mnamo mwezi Disemba.