1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Macron: Hatujaondoa uwezekano wa kutuma wanajeshi Ukraine

27 Februari 2024

Rais Macron amesema hawajaondoa uwezekano wa kutumwa kikosi cha wanajeshi wa mataifa ya Magharibi katika oparesheni za kijeshi za ardhini nchini Ukraine baada ya suala hilo kujadiliwa katika mkutano wa viongozi wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4cv42
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba wakati wa kufungua mkutano wa kujadili kadhia ya Ukraine
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba wakati wa kufungua mkutano wa kujadili kadhia ya UkrainePicha: Gonzalo Fuentes/AFP/Getty Images

Rais Emmanuel Macron amekataa kutoa maelezo juu ya mataifa ambayo yanafikiria kutuma wanajeshi wake nchini Ukraine.

Macron amewambia viongozi waliokusanyika mjini Paris kwamba watafanya kila linalowezekana kuizuia Urusi kushinda vita hivyo ambavyo vimeingia mwaka wake wa tatu sasa.

Rais huyo wa Ufaransa amewahimiza viongozi wa Ulaya kuhakikisha kile alichokiita "usalama wa pamoja" wa Ulaya kwa kuiunga mkono Ukraine hasa wakati huu ambapo inakabiliwa na mashambulizi makali ya Urusi.

Mkutano huo umehudhuriwa na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Poland Andrzej Duda pamoja na viongozi kutoka ukanda wa Baltic.