1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron akiri Ufaransa ingeliweza kuzuwia mauaji Rwanda 1994

Josephat Charo
4 Aprili 2024

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amekiri kuwa nchi yake na washirika wake wangeweza kukomesha mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 lakini walikosa ari ya kufanya hivyo.

https://p.dw.com/p/4eRPX
Emmanuel Macron
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anasema nchi yake na washirika wake walikosa ari ya kuzuwia mauaji ya kimbari ya Rwanda.Picha: ISAAC FONTANA/EPA/picture alliance

Ofisi ya Macron ilisema katika taarifa kwamba rais huyo wa Ufaransa atatoa ujumbe kwa njia ya video kupitia mitandao ya kijamii Jumapili ijayo, wakati Rwanda ikifanya kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji hayo.

Kwenye video hiyo, Macron anasema kwamba Ufaransa, ambayo ingeweza kuepusha mauaji hayo pamoja na washirka wake wa Magharibi na Afrika, ilikosa ari ya kufanya hivyo.

Soma zaidi: Paul Kagame: Shujaa au Dikteta?

Mnamo 2021, wakati wa ziara yake nchini Rwanda, rais Macron alitambuwa wajibu wa Ufaransa katika mauaji hayo ambapo watu 800,000 waliuawa, wengi wao wa jamii ya Tutsi na Wahutu waliojaribu kuwalinda.