1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LOME Rais mpya wa Togo, Faure Gnassingbe, ashindwa kujikwamua kutokana na lawama zinazomkabili.

18 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFcm

Rais mpya wa Togo, Faure Gnassingbe, ameshindwa kujikwamua kutokana na lawama za kunyakua madaraka ya kuliongoza taifa hilo. Viongozi barani Afrika na ulimwengu wote kwa jumla wamezilaumu juhudi za jeshi kumsaidia Gnassngbe kutawazwa kama rais mpya kufuatia kifo cha babake. Gnassingbe alisafiri hadi mjini Abuja, Nigeria kujitetea kwa kuchaguliwa kiongozi wa Togo kinyume cha sheria za nchi hiyo. lakini kiongozi huyo wa miaka 39 aliondoka mji wa Abuja baada ya kupewa onyo jipya na tishio la kuwekewa vikwazo. Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria, mwenyekiti wa umoja wa Afrika, anataka Togo ibadili hatua hiyo na kuitisha uchaguzi mkuu kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo.