1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura zaendelea kujumuishwa Zimbabwe

25 Agosti 2023

Wazimbabwe leo wanasubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi mkuu wakati ambapo maafisa kadhaa wa polisi wenye silaha na magari ya maji ya kuwasha wanakilinda kituo kikuu cha majumuisho ya kura.

https://p.dw.com/p/4VaPi
Wahlen in Simbabwe
Picha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe, ZEC, imesema bado inathibitisha matokeo kutoka kwenye vituo 12,500 vya kura na huenda ikaanza kutoa matokeo rasmi leo.

Matokeo ya kura ya rais yanatarajiwa kutolewa baada ya siku kadhaa.

Soma zaidi: Matokeo ya kwanza ya majimbo yatolewa Zimbabwe

Upigaji kura ulikamilika siku ya Alhamis (Agosti 24) baada ya usambazaji wa makaratasi ya kupigia kura kucheleweshwa katika mji mkuu, Harare, na kumfanya Rais Emmerson Mnangagwa kuongeza siku moja ya upigaji kura.

Mnangagwa, aliye na umri wa miaka 80, anawania kwa muhula wa pili ila anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Nelson Chamisa mwenye miaka 45.