1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Korea Kaskazini yatengeneza kombora jipya la masafa marefu

Saumu Mwasimba
12 Februari 2024

Shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini, KCNA limetangaza kwamba nchi hiyo imefanikiwa kutengeneza mfumo mamboleo wa kuzuia makombora ya masafa marefu.

https://p.dw.com/p/4cIUN
Korea Kaskazini | Kiwanda cha silaha
Kiwanda cha ujenzi wa silaha cha Korea KaskaziniPicha: Yonhap/picture alliance

Shirika hilo limeongeza kuripoti kwamba taasisi maalum inayohusika na shughuli za usimamizi wa utengenezaji makombora nchini humo imefanya ukaguzi wa majaribio ya mfumo huo wa ulinzi wa makombora ya masafa marefu jana Jumapili.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa, uwezo wa mfumo huo utatathminiwa tena  katika uwanja wa mapambano na katika kile kinachoitwa uboreshaji wa kasi wa kiufundi.

Soma pia:Korea Kaskazini yarusha makombora kadhaa baharini 

Hatua ya Kaskazini imekuja kufuatia majaribio kadhaa ya makombora ya nchi hiyo katika kipindi cha wiki za hivi karibuni pamoja na kuongezeka kwa ushirikiano kati ya serikali ya Pyongyang na Moscow, hatua ambayo imekosolewa na Marekani pamoja na washirika wake katika wakati ambapo mivutano imeongezeka katika rasi ya Korea.