1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Korea kaskazini na China zakubaliana kulinda maslahi yao

Tatu Karema
27 Januari 2024

Korea Kaskazini na China zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kimbinu na kutetea maslahi yao ya pamoja. Haya yameripoti na shirika la habari la Korea kaskazini KCNA

https://p.dw.com/p/4bjmK
Rais wa China Xi Jingping (kushoto) na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wakisalimiana kabla ya mazungumzo mjini Pyongyang mnamo Juni 20, 2019
Rais wa China Xi Jinping (kushoto) na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: Yonhap/picture alliance

Siku ya Ijumaa, China imesema kuwa imekubaliana na Korea Kaskazini kuimarisha mawasiliano ya kimkakati "katika ngazi zote" na kuthibitisha tena kuweko kwa msimamo usioyumba juu ya kuimarisha uhusiano huo wakati Sun alipokutana na mwenzake wa Korea Kaskazini, Pak Myong Ho, mjini Pyongyang.

Soma pia:China yataka mdahalo na Korea Kaskazini

Mkutano huo ni hatua ya hivi karibuni ya ushirikiano wa Korea Kaskazini na China pamoja na Urusi wakati ikiimarisha makabiliano yake na Marekani na Korea Kusini.

Soma pia:Xi ahimiza utatuzi wa amani wa suala la Korea Kaskazini

Korea Kaskazini imeimarisha kwa kiasi kikubwa uhusiano wake na mataifa hayo mawili ambayo ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na washirika wa jadi, ambayo yamesimama na nchi hiyo inapozidisha kasi yake ya utengenezaji wa silaha za kimkakati.