1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

Kongo: Mapigano yaendelea kati ya waasi wa M23 na Maimai

9 Oktoba 2023

Mapigano kati ya waasi wa kundi la M23 na vijana MaiMai wanaojiita Wazalendo huko Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameingia wiki yake ya pili baada ya kuripotiwa tena leo wilayani Rutshuru.

https://p.dw.com/p/4XIPs
Wapiganaji wa M23
Wapiganaji wa M23Picha: Guerchom Ndebo/AFP

Vyanzo mbalimbali vya ndani vimethibitisha kwamba mashambulizi hayo yalianza mapema asubuhi leo Jumatatu kutoka kwenye Milima ya Mulimbi na Kanaba  inayouzunguka mji huo wa TONGO.

Katika eneo hilo waasi wa M23 walizishambulia kwa mabomu ngome za vijana hao wajiitao Wazalendo kabla ya wao kujibu mashambulizi kwa kuvurumisha makombora kuelekea ngome za M23. 

Mwishoni mwa juma lililopita kushudiwa kwa mapigano makali baina ya pande zote mbili kurushiana risasikatika kijiji kidogo cha Kahunga, kilicho umbali wa kilomita tano kuelekea mji mkuu wa wilaya hiyo ya Rutshuru ambako pia kumetanda hali ya wasiwasi tangu jana hadi mchana huu. 

Soma pia:Muda wa M23 kusalimisha silaha wakamilika bila matunda

Raia kwenye maeneo hayo, ambayo yako kwenye dhamana ya majeshi la Kenya na Sudan Kusini chini ya Kikosi Maalum cha Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanasema wanaishi kwa hofu.

Raia na wakaazi wanavishutumu vikosi hivyo vya Afrika Mashariki kumeshindwa hadi sasa kurejesha utulivu.

Utulivu na amani vyatoweka kwa wiki mbili

Raia katika mji wa kimkamkati wa Kitshanga, mji mwingine unaoshuhudia machafuko kwa wiki nzima sasa, wameshuhudia hii leo asubuhi msururu wa vijana wajiitao Wazalendo wakipiga risasi angani kama ishara ya ushindi wao dhidi ya M23.

Demokratische Republik Kongo | Binnenvertriebene im Flüchtlingslager Kanyaruchinya
Pichani raia wakongo wakishuka katika gari la Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCRPicha: Aubin Mukoni/AFP/Getty Images

Kundi la waasi wa M23 waliuacha mji huo baada ya mapigano yaliyodumu kwa masaa kadhaa siku ya Jumapili.

Katika tangazo lao mwanzoni mwa wiki iliyopita, jeshi la Kongo lilikanusha madai kwamba linaunga mkono mapigano hayo kati ya vijana hao Wazalendo na waasi wa M23 wanaopoteza sasa baadhi ya ngome zao wilayani Masisi na Rutshuru.

Soma pia:Kongo yaomba jumuiya kimataifa kuwawekea vikwazo wahusika wa uvamizi wa Rwanda nchini humo

Kundi hilo linalolinyooshea kidole cha lawama jeshi la Kongo kuwa kwenye mstari wa mbele katika mapigano hayo limekuwa likitaka kufanyika mazungumzo ya moja kwa moja na serikali ya Kinshasa, ombi ambalo limetupiliwa mbali na utawala wa Rais Felix Tshisekedi. 

Uporaji wa mifugo, mazao ya mashamba pamoja nakuawa kwa raia wakawaida  ndio hali halisi ianayoshuhudiwa katika eneo zinazokumbwa na machafuko.

Muziki watumika kuhubiri amani Kongo