1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haniyeh asema hakuna mabadiliko katika mazungumzo ya Cairo

Bruce Amani
11 Aprili 2024

Kiongozi wa kisiasa wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh amesisitiza kuwa vifo vya watoto wake watatu wa kiume katika shambulizi la angani la Israel havitaathiri mazungumzo ya kusitishwa mapigano huko Gaza.

https://p.dw.com/p/4eev7
Ismail Haniyeh
Kiongozi wa kisiasa wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh Picha: Vahid Salemi/AP Photo/picture alliance

Israel imethibitisha mauaji hayo, ambayo yalitokea wakati mazungumzo mjini Cairo ya kusitishwa kwa muda mapigano na kuwachiwa mateka yakiendelea bila dalili za mafanikio.

Akizungumza na televisheni ya Qatar, Al Jazeera, Haniyeh amedokeza kuwa shambulizi hilo, ambalo pia liliwauwa wajukuu wake wanne, lilikuwa jaribio la kuubadilisha msimamo wa Hamas kuhusu mazungumzo hayo.

Haniyeh: Vifo vya wananagu Israel inajidanganya

Mazumgumzo yanayosimamiwa na Marekani, Misri na Qatar yamekuwa yakiendelea. Rais wa Marekani Joe Biden anasema Hamas inahitaji kufanya uamuzi wa haraka kuhusu pendekezo la karibuni la kusitishwa mapigano.

Wanamgambo hao wamesema wanalitathmini pendekezo hilo. Licha ya miito ya kusitishwa mapigano, Israel imeendelea leo na mashambulizi katika Ukanda wa Gaza na hasa kusini mwa eneo hilo.