1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kadima wajiondoa katika serikali ya Israel

18 Julai 2012

Chama kikuu katika serikali ya muungano ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kimejiondoa serikalini, kuhusiana na mzozo wa kuwabakisha nje Wayahudi wa madhehebu ya Orthodox katika usajili wa kijeshi

https://p.dw.com/p/15ZPh
Israel's Prime Minister Benjamin Netanyahu (L) speaks during a joint news conference with Shaul Mofaz, head of the Kadima party which will join Netanyahu's rightist coalition, at parliament in Jerusalem May 8, 2012. Netanyahu formed a unity government on Tuesday in a surprise move that could give him a freer hand to attack Iran's nuclear facilities and seek peace with the Palestinians. REUTERS/Ammar Awad (JERUSALEM - Tags: POLITICS)
Israel Premierminister Benjamin Netanjahu und Schaul MofasPicha: Reuters

Chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto, Kadima, kilijiondoa katika muungano wa serikali ya Netanyahu jana Jumanne, baada ya kupiga kura 25 kwa 3 kuondoka.

Kiongozi wake Shaul Mofaz aliwaambia kuwa hakuwa na budi ila kuvunja mkataba wa ushirikiano na chama cha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Likud, baada ya mazungumzo kuhusu sheria mpya ya huduma za jeshi kuvunjika.

Kuondoka kwa wabunge 28 wa Kadima kutamwacha Netanyahu katika uongozi wa serikali ya muungano na wingi mdogo wa viti 66 kati ya 120 bungeni, na kunaweza kuanzisha upya shinikizo la wabunge kupiga kura ya kulivunja bunge na kuandaa uchaguzi wa mapema kabla ya muda uliopangwa wa katika robo ya mwisho wa mwaka ujao.

Waziri wa mambo ya Kigeni wa Israel Avigdor Lieberman, asema atasalia serikalini
Waziri wa mambo ya Kigeni wa Israel Avigdor Lieberman, asema atasalia serikaliniPicha: picture-alliance/dpa

Chama cha Kadima kilijiunga na serikali ya muungano mwezi Mei, baada ya kuondoa uwezekani wa kufanyika uchaguzi wa mapema, katika mojawapo ya mishangao mikubwa zaidi katika historia ya siasa za Israel za nyakati za hivi karibuni.

Lakini vyama hivyo viwili vimeshindwa kuelewana kuhusiana na kuidhinisha sheria ya kuchukua nafasi ya ile ambayo iliwawacha nje wanafunzi wa madhehebu ya Orthodox dhidi ya kujiunga jeshini, lakini ambayo Mahakama Kuu iliiondoa mwezi Februari.

Athari mbaya kwa mchakato wa amani

Hata ikiwa Netanyahu atafaulu kuuiweka pamoja serikali yake ya muungano iliyoathirika, mzozo huu wa kighafla ina athari mbaya kwa mchakato wa amani ya mashariki ya kati, na kumwacha na wabunge walio na misimamo mikali na wanaopinga makubaliano yoyote na Wapalestina. kiongozi wa chama cha Kadima Shaul Mofaz, alisema walijaribu kufikia makubaliano kuhusu sheria hiyo lakini hilo halikufanikiwa, akiongeza kuwa wanaondoka kiujasiri kwenda kuongoza nchi wakiwa upande wa upinzani.

Netanyahu alitaka mfumo ambao ungesajili taratibu idadi inayoendelea kuongozeka ya wanafunzi Wayahudi wa madhehebu ya Orthodox, kwa miaka kadhaa, na kuendelea kuwawacha nje idadi ndogo yao. Katika barua aliyomwandikia Mofaz, Netanyahu alielezea masikitiko yake kuhusiana na uamuzi wa Mofaz.

Waziri wa mambo ya Kigeni wa Israel Avigdor Lieberman, asema atasalia serikalini
Waziri wa mambo ya Kigeni wa Israel Avigdor Lieberman, asema atasalia serikaliniPicha: picture-alliance/dpa

Haijabainika wait kitakachofanyika baada ya tarehe mosi Agosti. Waziri wa Ulinzi Ehud Barak alisema, tarehe hiyo ikifika ataanza kuwasajili wanajeshi wa kidini wa kiasi kisichojulikana na kupendekeza sheria ya muda hadi mpango wa kudumu zaidi utakapofikiwa katika miezi ijayo.

Watalaamu wa mambo ya siasa wanadai kuwa Waziri Mkuu wa zamani Ehud Olmert, aliyefutiwa kesi ya ufisadi wiki iliyopita, huenda akarejea katika siasa. Profesa wa Masuala ya siasa Yaron Ezrahi kutoka chuo kikuu cha Kiyahudi anasema Netanyahu atatuliza kimbunga hicho.

Anasema baada ya mazungumzo ya amani kukwama chini ya utawala wa miaka mitatu wake Netanyahu, sasa Waziri huyo Mkuu ataendelea kushirikiana na Marekani ili kuizuia Iran dhidi ya kutengeneza silaha za nyuklia, suala ambalo linaungwa mkono na umma.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters/AP
Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman