1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, mzozo wa njaa unaweza kuepukika nchini Ethiopia?

5 Februari 2024

Ukame, mizozo na ufisadi, baadhi ya sababu za mzozo wa njaa unaoikumba Ethiopia ambazo ni tofauti na zinazoweza kuepukika. Lakini wakati Waethiopia wakilala njaa, wanasiasa wanaendelea kuzishibisha njaa zao za madaraka.

https://p.dw.com/p/4c4ee
 Ethiopia I mzozo wa njaa Tigray
Ugawaji wa chakula cha msaada AmharaPicha: Eduardo Soteras/AFP

Mwaka 1985 mwanamuziki na mwanaharakati bob Geldof aliandaa matamasha ya muziki kwa ajili ya msaada katika miji ya London na Philadelphia ili kuchangisha fedha kwa ajili ya ukame wa miaka miwili uliokuwa umeikumba Ethiopia.

Baa la njaa: Uko wapi umoja wa Afrika?Karibu miongo minne baadae, huenda Geldof ambaye amestaafu akahitajika kurudi tena na kuandaa tamasha jengine iwapo makadirio na hesabu za wataalam wa masuala ya njaa Ethiopia zitakuwa kweli.

Kulingana na Shirika la Chakula Duniani WFP, watu milioni 20 Ethiopiawanahitaji msaada wa chakula.

Msaada wa chakula Ethiopia
Lori la mpango wa chakula duniani WFPPicha: Alemenew Mekonnen/DW

Mkuu wa zamani wa WFP ambaye hataki kutajwa ameliambia shirika la habari la Associated Press AP kwamba nchi hiyo ya Pemba ya Afrika inaelekea katika ukosefu wa chakula kwa mara nyengine.

Getachew Reda, rais wa utawala wa mpito jimboni Tigray hivi majuzi alisema zaidi ya asilimia 90 ya idadi ya watu katika eneo hilo wako kwenye hatari ya kukumbwa na ukosefu wa chakula na kifo. Mamlaka za Tigray zimeonya kuwa ukosefu wa chakula uliopo sasa unaweza kukifikia kiwango kile kilichoshuhudiwa kati ya mwaka 1984 na 1985 ambapo mamia kwa maelfu ya watu walifariki dunia.

Lakini serikali mjini Addis Ababa awali ilikuwa ikijaribu kuzipuuza ripoti hizi kama zisizo sawa na kumtuhumu reda kwa kuutilia siasa mzozo huo.WFP yaanza kusambaza tena chakula Ethiopia

Mwaka 2022, kikosi cha Umoja wa Mataifa kilichapisha ripoti iliyoituhumu serikali ya Ethiopia kwa kutumia njaa kama silaha, miongoni mwa ukiukaji mwengine wa haki za binadamu wakati wa mzozo wa Tigray.

Akifahamu kwamba katika miaka ya nyuma serikali ya nchi hiyo haikukabiliana vyema na matatizo ya njaa, Waziri Mkuu Abiy Ahmed alirudi chini kidogo hivi majuzi na kwa pamoja akatoa taarifa ya pamoja na Umoja wa Mataifa, akisema watu wa eneo hilo la Tigray bado hawajarudi katika hali ya kawaida kutokana na mapigano yaliyokwisha.

Sasa baada ya miaka ya mapigano makali, serikali taratibu inakiri kwamba watu wa Tigray na Amhara wanakabiliwa na adui mpya, njaa.

Ethiopia
Watu walioathirika na njaa mkoani TigrayPicha: Million Hailesilassie/DW

Takwimu za hivi majuzi zinaonyesha kwamba karibu watu 372 tayari wamefariki dunia kama athari ya njaakatika miezi sita iliyopita katika eneo lenye ukosefu wa usalama la kaskazini mwa nchi hiyo.

Ukosefu wa chakula umeongezeka sababu ikiwa vita katika jimbo la Tigray na machafuko katika jimbo jirani la Amhara na ukosefu mbaya wa mvua kuwahi kushuhudiwa katika Pembe ya Afrika kwa miongo kadhaa, umeizidisha hali hiyo, hasa Tigray.Asilimia 40 ya watu wa Tigray wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula

Laetitia Bader ni naibu mkurugenzi wa shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch HRW na aliiambia DW,

"Hakuna shaka kwamba mzozo mzozo na ukame vinahusiana kwa sasa kaskazini mwa Ethiopia na kuchangia katika hali mbaya ya ukosefu wa usalama wa chakula huko."Ukame Pembe ya Afrika wasababisha njaa kwa watu milioni 13

Kulingana na Umoja wa Mataifa, ukosefu wa usalama unaoendelea katika eneo hilo katika masuala ya kisiasa na changamoto za kilimo ni mambo yanayomaanisha kwamba ni nusu ya mashamba ya Tigray tu yaliyotumika katika msimu mkuu wa upanzi mwaka jana. Fauka ya hayo, ni kama thuluthi moja tu ya mazao yaliyoweza kutumika. Katika baadhi ya maeneo huko Tigray, mazao yaliripotiwa kuwa chini ya asilimia mbili.

Madhila ya njaa Tigray baada ya vita

Mnamo mwezi Machi 2023 shirika la WFP liliamua kusitisha usambazaji wa misaada ya chakula jimboni Tigray kwasababu ya ripoti za wizi wa chakula hicho hasa nafaka. Baadae, shirika hilo la Umoja wa Mataifa liliyaongeza marufuku hayo kuwa ya Ethiopia nzima kutokana na ufisadi uliokithiri katika kusambaza misaada ya chakula.UN yaonya kuwa raia wa Tigray wanakabiliwa na kitisho cha njaa

Haijabainika wazi ni nani aliyenufaika na wizi huo wa misaada ila baadhi ya makundi ya kutoa misaada ya kiutu yanawalaumu maafisa wa serikali huku baadhi wakilinyonesha kidole cha lawama jeshi la nchi hiyo lenye nguvu.

Lakini miezi sita iliyopita tu, WFP lilianza tena kusambaza misaada nchini Ethiopia ingawa ni watu wachache tu Tigray wanaosema kwamba wanapokea misaada ya chakula.UN: Watu milioni 13 wanakabiliwa na njaa kubwa katika eneo la Pembe ya Afrika

Ila yote haya yakifanyika, kinaya ni kwamba Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed hivi majuzi huko nchini Italia, alituzwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula la Kilimo FAO tuzo ya Agricola, ambayo ndiyo tuzo ya juu kabisa anayoweza kupewa mtu na shirika hilo.

FAO ilisema imetambua maono, uongozi na dhamira ya Abiy katika masuala ya usalama wa chakula.