1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ivory Coast mabingwa AFCON 2024

Sudi Mnette
12 Februari 2024

Ivory Coast jana imeandika historia baada ya kujinyakulia taji la ubingwa wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON kwa kuitwanga Super Eagles ya Nigeria mabao 2-1.

https://p.dw.com/p/4cHX2
Kandanda | Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika | Mshindi Ivory Coast
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara (katikati) akinyanyua taji la Kombe la Mataifa ya Afrika kwenye jukwaa baada ya Ivory Coast kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika.Picha: FRANCK FIFE/AFP

Nigeria ndio ilikuwa ya kwanza kufungua lango la mwenyeji wake baada ya kufunga bao safi kabisa katika dakika ya 38 ya kipindi cha kwanza na mchezaji, William Troost-Ekong. Lakini baadae katika kipindi cha pili mambo yakabadilika. Franck Kessié Ivory Coast aliliona lango la hasimu wake kunako dakika ya 62 na dakika 81 Sébastien Haller akatoa hakikisho la bao la ushindi kwa timu hiyo. Hii ni mara ya tatu kwa Ivory Coast kulitwaa Kombe laAFCON baada ya kuchukua ubingwa mwaka 1992 na  mara ya mwisho ikawa 2014.