1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yafanya mashambuzi makali kusini mwa Gaza

Sudi Mnette
2 Desemba 2023

Jeshi la Israel leo hii limeyalenga maeneo ya kusini mwa Ukanda wa Gaza, na kuzidisha mashambulizi mapya baada ya kumalizika kwa mapatano ya kusitisha mapigano yaliodumu kwa juma moja kati yake na Hamas.

https://p.dw.com/p/4Zhhx
Mashambulizi mapya huko Gaza baada ya kumalizika kwa mapatano ya kusitisha mapigano yaliodumu kwa juma moja kati Israel na Hamas
Mashambulizi mapya huko Gaza baada ya kumalizika kwa mapatano ya kusitisha mapigano yaliodumu kwa juma moja kati Israel na HamasPicha: AFP

Hatua hii inazusha wasiwasi mwingine kuhusu vifo vya raia. Mashambulizi mengi ya Israeli ya sasa yalilenga mji wa Khan Younis ulioko kusini mwa Gaza, ambapo jeshi limesema limeyalenga maeneo 50 ya Hamas kwa mashambulizi ya ndege, vifaru na jeshi la majini.

Jeshi la Israel lilidondosha vipeperushi vya kutoa onyo kwa wakazi kuondoka katika eneo hilo hadi jana Ijumaa jioni. Lakini kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa hakukuwa na taarifa ya idadi kubwa ya watu kuondoka.

Jeshi la Israel limesema pia kuwa limefanya mashambulizi Gaza Kaskazini, na kwamba limepiga jumla ya maeneo 500 kote katika Ukanda wa Gaza.

Wizara ya afya ya Gaza imeripoti kuwa watu wasiongua 200 wameuawa tangu kuanza tena kwa mashambulizi mapya.