1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaJapan

Idadi ya vifo yaongezeka na kufikia 161 nchini Japan

8 Januari 2024

Idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililoipiga Japan siku ya Mwaka Mpya imeongezeka hadi kufikia watu 161.

https://p.dw.com/p/4axW8
Japan Erdbeben Aufräumarbeiten
Vikosi vya uokoaji vikiendelea kuwasaka waathiriwa wa tetemeko hilo katika mji wa Suzu, Ishikawa: 07.01.2024Picha: The Yomiuri Shimbun via AP /picture alliance

Kulingana na mamlaka katika mkoa wa kati wa Ishikawa, idadi ya watu ambao hawajulikani waliko imepungua hadi 103 kutoka 195.

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.6 katika kipimo cha Richter liliikumba miji ya Toyama, Ishikawa na Niigata, yote ikiwa kwenye kisiwa kikubwa cha Honshu kilicho kwenye mwambao wa magharibi wa  Bahari ya Japan . Baadaye Mamlaka ya hali ya hewa ilitoa onyo la kutokea tsunami kubwa.

Daima nchini humo, safari za ndege zimerejea kama kawaida leo Jumatatu katika uwanja wa ndege wa Tokyo wa Haneda, siku sita baada ya kutokea ajali ya ndege mbili kugongana na kusababisha vifo vya watu watano.