1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC yaanza mchakato wa kesi ya Kony

Tatu Karema
26 Februari 2024

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imeanzisha mchakato wa kusikiliza kesi dhidi ya kiongozi wa kundi la waasi la Lord Resistance Army (LRA) nchini Uganda, Jopseph Kony, licha ya kuwa hajakamatwa hadi leo.

https://p.dw.com/p/4cuCs
Lord Resistance Army ya Uganda
Kiongozi wa kundi la waasi wa LRA nchini Uganda, Joseph Kony (kushoto) akiwa na msaidizi wake, Vincent Otti.Picha: Stuart Price/dpa/picture alliance

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama hiyo, Karim Khan, aliye ziarani nchini Uganda amekutana na kushauriana na taasisi za kisheria nchini humo pamoja na Rais Yoweri Museveni kuhusu hatua hiyo.

Ikielekea kufunga kesi ya muda mrefu dhidi ya viongozi wa LRA, ICC imeamua kuendesha kesi dhidi ya Kony bila uwepo wake kama njia ya kuhakikisha haki inatendeka na pia waathiriwa wanapata fidia.

Waasi wa LRA wanaelezewa kutenda uhalifu dhidi ya binaadamu kaskazini mwa Uganda na pia katika mataifa jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini.

Maovu hayo yalifanywa na waasi hao takriban miaka 20 iliyopita, ingawa ni makamanda wawili tu kati ya watano wa LRA walioorodheshwa na ICC ambao walikamatwa kuhusiana na vitendo vyao.