1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hermoso akanusha kutoa ridhaa ya kupigwa busu na Rubiales

Sylvia Mwehozi
26 Agosti 2023

Kikosi cha mabingwa wa dunia cha wanawake cha Uhispania kimetishia kutocheza tena endapo mkuu wa shirikisho la soka la nchi hiyo RFEF Luis Rubiales hatojiuzulu.

https://p.dw.com/p/4VbIj
Jennifer Hermoso Fuentes
Jenni Hermoso mchezaji wa soka wa timu ya Uhispania ya wanawakePicha: Noe Llamas/ZUMAPRESS/picture alliance

Kikosi cha mabingwa wa dunia cha wanawake cha Uhispania kimetishia kutocheza tena endapo mkuu wa shirikisho la soka la nchi hiyo RFEF Luis Rubiales hatojiuzulu.

Rubiales amekataa kujiuzulubaada ya kutuhumiwa kwa wiki nzima kufuatia hatua yake ya kumbusu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake Jenni Hermoso baada ya ushindi wao wa Kombe la Dunia.

Baadae mchezaji huyo alikanusha kwa hasira madai ya Rubiales kwamRubiales atakiwa kuomba msamaha kwa kumbusu Hermosoba alitoa ridhaa ya kupigwa busu. Baraza la juu la michezo la Uhispania CSD limetangaza kwamba linalenga kumsimamisha kazi.

Rubiales atakiwa kuomba msamaha kwa kumbusu Hermoso

Shirikisho la soka duniani FIFA lilianzisha uchunguzi wa kimaadili kuhusu tukuio hilo huku chama cha wachezaji FIFPRO kikishinikiza shirikisho la soka Ulaya UEFA, nalo kuchukua hatua kama hiyo. Rubiales ni miongoni mwa makamu wa rais wa UEFA.