1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boeing kufidia familia za wahanga wa ajali ya Ethiopia

11 Novemba 2021

Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing imefikia makubaliano na familia za wahanga wa ajali ya ndege ya 737 MAX iliyowauwa watu 157 nchini Ethiopia.

https://p.dw.com/p/42riU
Deutschland Berlin Boeing 787 Dreamliner
Picha: picture-alliance/dpa/R. Schlesinger

Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing imefikia makubaliano na familia za wahanga wa ajali ya ndege ya 737 MAX iliyowauwa watu 157 nchini Ethiopia. Boeing imekubali kuwajibikia mkasa huo, kwa mujibu wa nyaraka za kisheria zilizowasilishwa katika mahakama moja ya Chicago jana. Taarifa ya kampuni hiyo imesema Boeing imedhamiria kuhakikisha kuwa familia zote za waliopoteza wapendwa wao katika ajali za ndege zao wanafidiwa kikamilifu na kwa haki kufuatia matukio hayo. Kwa kukubali kuwajibika, makubaliano hayo ya Boeing na familia hizo yanaziwezesha pande zote kuangazia juhudi za kuamua fidia inayostahili kwa kila familia. Ndege ya shirika la Ethiopia namba 302 kuelekea Nairobi, ilianguka kusini mashariki mwa mji mkuu Addis Ababa dakika sita baada ya kupaa mnamo Machi 10, 2019.