1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken ziarani Afrika kupunguza ushawishi wa Urusi

Mohammed Khelef
24 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken yupo barani Afrika kuinadi Marekani kuwa ni mshirika bora wa nchi za eneo la Sahel, badala ya kundi la mamluki wa Urusi la Wagner.

https://p.dw.com/p/4bcMF
Antony Blinken na José Ulisses de Pina Correia e Silva
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken (kushoto) akiwa na Waziri Mkuu wa Cape Verde, José Ulisses de Pina Correia e Silva.Picha: Ângelo Semedo/DW

Waziri Blinken anayeitembelea Nigeria, katika ziara yake ya barani Afrika, amesema Marekani ipo tayari kuendelea kuisaidia Nigeria na washirika wengine katika juhudi za kuleta utulivu kwenye eneo la Sahel, ambalo limegeuzwa kuwa uwanja hatari wa kigaidi, baada ya mapinduzi kadhaa ya kijeshi kufanyika hivi karibuni.

Blinken amesema mjini Abuja kwamba maendeleo yatapatikana kwa kurejesha utawala wa kikatiba, kwa ushirikiano wa nchi za ukanda wa Sahel na Marekani katika kuleta usalama.

Amesema Nyanja muhimu ya msaada wa Marekani kwa Nigeria na nchi nyingine za ukanda wa Sahel ni kuimarisha uwezo wa majeshi ya usalama kwa njia ya vitendea kazi, tekinolojia na kupeana taarifa za kijasusi.