1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yaionya Marekani juu ya masuala hasi baina yao

Lilian Mtono
26 Aprili 2024

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na wa China Wang Yi wamekutana hii leo mjini Beijing katika mazungumzo yatakayoangazia changamoto kadhaa baina yao.

https://p.dw.com/p/4fCSv
China, Beijing | Antony Blinken akutana na Wang Yi
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinke(kushoto) na Wang Yi(kulia) wakipeana mikono wakati wa mkutano mjini BeijingPicha: Mark Schiefelbein/POOL/AFP/Getty Images

Blinken na wasaidizi wake walianza mazungumzo hayo siku moja baada ya mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu kuziomba Marekani na China kusuluhisha tofauti zao kwa kuzingatia uwajibikaji.

Blinken atatumia masaa kadhaa na Wang kwenye mikutano ya ndani ili kujaribu kusuluhisha tofauti zao huku madai ya kwamba China inaisaidia Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine, likitarajiwa kuibuliwa. 

Kwenye ufunguzi wa mikutano hiyo, Wang amemwambia Blinken kwamba uhusiano wa China na Marekani umeimarika, ingawa masuala hasi pia yanazidi kuongezeka.