1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bin Salman akutana na waziri wa mambo ya nje wa Iran

18 Agosti 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hossein Amir Abdollahian amekutana na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman leo.

https://p.dw.com/p/4VKZD
Hossein Amir-Abdollahian amepokelewa na mwenyeji wake Bin Salman katika mji wa Bahari ya Shamu wa Jeddah.
Hossein Amir-Abdollahian amepokelewa na mwenyeji wake Bin Salman katika mji wa Bahari ya Shamu wa Jeddah.Picha: Fars

Shirika rasmi la habari nchini Saudi Arabia SPA limeripoti kuwa mwanamfalme huyo amempokea waziri huyo wa mambo ya nje katika mji wa Bahari ya Shamu wa Jeddah, ambapo wamejadiliana kuhusiana na mahusiano ya nchi zao mbili na uwezekano wa fursa za kushirikiana katika siku zijazo.

Shirika la habari la SPA vile vile limeripoti kuwa viongozi hao wawili wamejadili pia maendeleo ya hivi karibuni ya kikanda na kimataifa.

Hii ndio ziara ya kwanza ya Abdollahian nchini Saudi Arabia tangu nchi hizo mbili zinazohasimiana kikanda, kukubali kuwa na mahusiano mema tena baada ya mpasuko uliodumu kwa mwaka mzima.

Hapo jana Abdollahian alifanya mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Saudia, Faisal bin Farhan.