1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge Uingereza lauchelewesha mpango wa wakimbizi wa Sunak

Amina Mjahid
23 Januari 2024

Baraza la juu la bunge la Uingereza limepiga kura kuuchelewesha mpango wenye utata wa serikali wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda.

https://p.dw.com/p/4ba6B
England London | Rishi Sunak
Kucheleweshwa kura hiyo ni pigo kwa Waziri Mkuu Rishi SunakPicha: James Manning/AP/picture alliance

Hatua hiyo ni pigo kubwa kwa Waziri Mkuu Rishi Sunak, aliyeliomba baraza hilo kuupitisha mpango huo, akisema ndio matakwa ya Waingereza walio wengi.

Kura 214 kati 171 zilipigwa kuuchelewesha mpango huo uliotiwa saini kati ya Uingereza na Rwanda, hadi pale serikali ya Uingereza itakapoonesha na  kwamba Rwanda ni mahala salama kwa wahamiaji watakaoondolewa kutoka Uingereza.

Soma pia: Sunak apata "pigo" katika kuwapeleka wahamiaji Rwanda

Mpango huo ni muhimu kwa serikali ya kihafidhina ya Rishi Sunak, kudhibiti uhamiaji haramu, kwa kuwapeleka waomba hifadhi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.