1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock yuko ziarani nchini Macedonia Kaskazini

23 Machi 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anataka kupiga chapuo zaidi hatua za Macedonia Kaskazini katika mpango wake wa kujiunga katika Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4P70T
Nord-Mazedonien Annalena Baerbock in Skopje
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock (kushoto) akiwa pamoja na mwenzake wa Macedonia Kaskazini Bujar Osmani kwenye mji mkuu wa taifa ilo Skopje.Picha: Petr Stojanovski/DW

Baerbock amewasili nchini humo leo hii na mkutano kati yake na mwenziwe Bujar Osmani umepangwa kufanyika asubuhi hii katika mji mkuu Skopje. Baadae, amepanga kukutana na wawakilishi wengine wa serikali, upinzani na bunge.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani taifa hilo la Balkan ya Magharibi, ni nchi muhimu katika mchakato wa upanuzi wa mipaka ya Umoja wa Ulaya.