1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afya ya uzazi bado ni changamoto kwa mataifa mbalimbali

Salma Said11 Novemba 2022

Viongozi walioshiriki katika uzinduzi wa ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya Nairobi uliofanyika visiwani Zanzibar, wameeleza kuwa pamoja na jitihada zinazoendelea bado afya ya uzazi ni changamoto.

https://p.dw.com/p/4JNWh
Benin I Gesundheit I Frauen
Picha: Delphine Bousquet/AFP/Getty Images

Wito huo umetolewa na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete katika uzinduzi wa ripoti hiyo maalumu, juu ya utekelezaji wa maazimio ya Nairobi yaliyowekwa mwaka 2019 ambapo maazimio 12 yalionekana ndio muhimu zaidi na yanahitaji utekelezaji.

Spanien Schwangere Frau
Afya ya mama mjamzito bado iko mashakaniPicha: picture-alliance/empics/PA Wire/Y. Mok

Akizungumza katika mkutano huo Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi ambaye alikuwa mweyeji wa mkutano alisema kwa msaada wa washirika wa maendeleo Serikali yake inaendelea kuandaa mfumo wa afya, kujenga miundo mbinu ya Afya , kuajiri rasilimali watu, sambamba na kupata vifaa tiba zaidi za afya ili kutoa huduma bora za afya mijini na vijijini.

Kamisheni ya ufuatiliaji wa maazimio ya Nairobi yenye makamishna 27 na wenyeviti wenza wawili Jakaya Kikwete na Michaelle Jeans. Kazi ya kamisheni hiyo imechukua miaka mitatu kufuatilia utekelezaji wa kazi hiyo.