1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nahodha wa Bafana Bafana auawa kwa kupigwa risasi

28 Oktoba 2014

Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Afrika Kusini na nahodha wa timu hiyo Senzo Meyiwa amepigwa risasi na kufariki katika tukio la uporaji karibu na jiji la Johannesburg siku ya Jumapili

https://p.dw.com/p/1Dd5G
Senzo Meyiwa Torhüter Südafrika
Picha: Lefty Shivambu/Gallo Images/Getty Images

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyekuwa akichezea timu ya Orlando Pirates alifariki jana baada ya kupigwa risasi moja kifuani nyumbani kwa mpenzi wake Kelly Khumalo, mcheza sinema na mwimbaji , katika kitongoji cha Vosloorus mjini Johannesburg.Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma leo amewaongoza wananchi wa taifa hilo lililojawa na simanzi kutokana na kifo cha nahodha wa Bafana Bafana Senzo Meyima.

Watu wengi ikiwa ni pamoja na mashabiki wa timu ya Orlando Pirates wamekusanyika katika eneo la tukio wakiomboleza kifo cha mlinda mlango huyo maarufu nchini Afrika kusini. Mmoja wa mashabiki hao amesema. "Niko hapa kama mpenzi wa Pirates. Nataka kuwa hapa ambapo mlinda mlango wetu wa kwanza amepoteza maisha. Na uhalifu huu kwa jumla unaiathiri nchi yetu. Kupoteza vijana kama hawa wakiwa katika wakati wa kilele cha maisha yao ya uchezaji kandanda , kwa kweli sio sahihi".

Polisi imesema jana kuwa watu wawili waliingia katika nyumba ya Kelly Khumalo usiku, mmoja alibakia nje ya nyumba na wote watatu walikimbia mara baada ya tukio hilo. Meyiwa akifariki wakati alipofikishwa hospitalini, polisi wameongeza.

Senzo Robert Meyiwa Torhüter Südafrika
Senzo Robert Meyiwa aokoa kombora wakati wa mchuano wa kirafiki dhidi ya AustraliaPicha: picture-alliance/AP Photo/Rick Rycroft

"Tunawahakikishia Waafrika kusini wote kwamba tutafanya kila linalowezekana kuwafikisha wauaji wa Meyiwa katika sheria , imesema taarifa ya polisi ya Afrika kusini katika ukurasa wa Tweeter na kutoa zawadi ya dola 13,700 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa za wahalifu hao.

Kocha wa timu ya taifa ya Afrika kusini Ephraim Mashaba amewapa pole wachezaji kadhaa waliokuwa wakicheza na Meyiwa ambao wamewasili hospitalini hapo muda mfupi baada ya shambulio hilo.

Zaidi ya watu 17,000 wameuwawa nchini Afrika kusini kati ya Aprili 2013 na Machi 2014 , ikiwa ni ongezeko la kiasi ya watu 800 kutoka idadi ya mwaka uliopita, kwa mujibu wa tarakimu za polisi.

Kocha wa Cameroon Volker Finke amekiri katika mahojiano yaliyochapishwa leo kuwa anashangaa kwa kutofutwa kazi baada ya matokeo mabaya katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka huu, lakini hivi sasa anamatumaini ya kuingia katika changamoto mpya.

Nayo ligi ya Afrika kusini imeahirisha mchezo wa watani wa jadi mwishoni mwa juma hili kati ya Orlando Pirates ya Soweto na Kaiser Chiefs baada ya kifo cha mlinda mlango huyo wa Pirates na timu ya taifa Senzo Meyiwa.

Tume ya maadili ya kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC imewasiliana na rais wa shirikisho la tennis nchini Urusi Shamil Tarpiechev kujieleza kuhusu matamshi yake juu ya Venus na Serena Williams kuwa ni kaka wawili badala ya dada wawili, na kuongeza kuwa wanatisha kuwaangalia. Alitoa matamshi hayo katika televisheni. matamshi hayo yamesababisha rais huyo wa shirikisho la Tennis nchini Urusi kupigwa faini na kuzuiwa kushiriki katika michezo ya tennis ya wanawake duniani.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / ZR / afpe
Mhariri: Yusuf , Saumu