1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya kutafuta amani nchini Kenya

25 Juni 2014

Kiasi ya watu ishirini waliuawa siku ya Jumapili katika eneo la Wajir kaskazini mashariki mwa Kenya kufuatia mapigano makali kati ya makabila hasimu katika eneo hilo linalopakana na Somalia.

https://p.dw.com/p/1CPmi
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Rais Uhuru Kenyatta wa KenyaPicha: picture-alliance/AA

Kulingana na umoja wa Mataifa, kiasi ya watu 75,000 wameyatoroka makaazi yao katika miji ya Wajir na Mandera huku wengine 60,000 wakiathirika na mapigano hayo ya kikabila. Hapo jana viongozi wa kutoka eneo hilo walikutana na rais Uhuru Kenyatta kuzungumzia hali hiyo. Caro Robi amezungumza na mmoja wa washiriki wa mazungumzo hayo ya kutafuta amani Ugas Sheikh na kwanza ametaka kujua iwapo hali ya utulivu imerejea katika eneo hilo. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mhariri: Caro Robi

Mwandishi: Mohammed AbdulRahman