1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya kura yasubiriwa Tunisia

mjahida24 Novemba 2014

Kura zinaendelea kuhesabiwa Tunisia, katika uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu kuondolewa madarakani, rais wa miaka mingi Zine El Abidine Ben Ali katika maandamano ya umma mwaka wa 2011.

https://p.dw.com/p/1Ds8L
Wagombea wakuu wa uchaguzi Tunisia Beji Caid Essibsi na Moncef Marzouki.
Wagombea wakuu wa uchaguzi Tunisia Beji Caid Essibsi na Moncef Marzouki.

Upigaji unaendelea katika baadhi ya maeneo nchini humo huku pia shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea. Muda mfupi baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa jana Jumapili, washirika wa aliyekuwa Waziri Mkuu Beji Caid Essibsi – anayetokea chama kisichofungamana na dini cha Nidaa Toune walidai Beji anaongoza dhidi ya mpinzani wake rais wa mpito Moncef Marzouki.

Hata kablya ya matokeo rasmi mmoja ya washirika wake Mohsen Marzouk aliwashukuru wapiga kura kwa kuonesha uaminifu wao kwa mgombea Beji Caid Essebi

"Bwana Beji Caid Essebsi, kulingana na matokeo ya mwanzo ndio wa kwanza katika kinyanganyiro hiki akiwa akimuacha mbali mpinzani wake. Na tunataka kuwashukuru watu wa Tunisia kwa imani yao," alisema Mohsen Marzouk.

Mmoja wa washirika wa Beji Mohsen Marzouk
Mmoja wa washirika wa Beji Mohsen MarzoukPicha: picture alliance/AA/A. Landoulsi

Nayo Televisheni ya Kitaifa ya Tunisia 1 ilionyesha matokeo ambayo sio rasmi yakimuonesha Essibsi akiwa na takriban asilimia 48 ya kura akiliganishwa na Moncef Marzouki aliyeonekana kuwa na asilimia 27 ya kura.

Hata hivyo akizungumza na waandishi habari baada ya kumalizika zoezi la kupiga kura, Marzouki alisema yuko tayari kukubali matokeo ya kura yanayotarajiwa kutolewa rasmi siku ya Jumanne.

Duru ya pili ya uchaguzi huenda ikafanyika mwishoni mwa Desemba

Aidha takriba wagombea 27 walishiriki katika uchaguzi huu na iwapo hapatakuwa na mgombea yeyote atakayefikisha asilimia inayohitajika ili kutangazwa rais basi wagombea wawili watakaokuwa wanaongoza kwa kura wataingia katika duru ya pili ya uchaguzi tarehe 28 Desemba.

Wakati huo huo baadhi ya wapiga kura walielezea kuwa na hamu ya kushiriki katika uchaguzi ambao ni hatua muhimu kuelekea katika demkokrasia ya Tunisia." Hii ni mara ya kwanza nimepiga kura na kumchagua rais, sitaki mtu anayetokea katika utawala wa Ben Ali kushika nafasi hii nataka rais aliyeshiriki katika maandamano ya kutaka mageuzi," alisema Hajer mwanamke aliyeshiriki katika uchaguzi huo.

Awali mkuu wa tume huru ya uchaguzi nchini humo Shafiq Sarsar alisema takriban asilimia 54 ya watu millioni 5.2 walipiga kura nchini humo huku akisisitiza kuwa zoezi la upigaji kura liliendeshwa kwa amani bila ya kuwepo visa vya ghasia.

Wafanyakazi wa tume ya uchagfuzi wakiendelea na zoezi la kuhesabu kura.
Wafanyakazi wa tume ya uchagfuzi wakiendelea na zoezi la kuhesabu kura.Picha: Reuters/Z. Souissi

Lakini kwa upande wao waangalizi wa uchaguzi wameripoti kuwepo kwa visa vya ununuzi wa kura na hata majaribio ya kuwashawishi wapiga kura huku waangalizi wa ulaya wakisema uchaguzi umefanyika vizuri ukilinganishwa na uchaguzi wa bunge uliofanywa mwezi uliopita.

Kulingana na katiba ya Tunisia iliopitishwa mwaka huu inampa madaraka makubwa Waziri Mkuu kuliko rais wan chi ambaye anayeshughulika na mambo ya nje pamoja na ulinzi. Rais atakayepatikana kupitia uchaguzi huu atakabiliwa na changamoto ya kurejesha tena usalama ambapo washukiwa wa kundi lililo na itikadi kali wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama katika miezi ya hivi karibuni.

Mwandishi: Amina Abubakar/AFP/Reuters

Mhariri: Yusuf Saumu