1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yatumbukiza mabao manane dhidi ya Hamburg

16 Februari 2015

Bayern Munich yapikisha mipira mara nane wavuni mwa Hamburg SV, Borussia Dortmund yaondoka kwa mara ya kwanza tangu mwaka kuanza kutoka katika eneo la hatari ya kushuka daraja.

https://p.dw.com/p/1EcWJ
Fußball Bundesliga 21. Spieltag FC Bayern vs. Hamburger SV
Bayern Munich waangusha mvua ya magoli dhidi ya Hamburg SVPicha: Alexander Hassenstein/Bongarts/Getty Images

Ulikuwa mchezo kama wa majaribio usiokuwa na upinzani unaoonekana katika ligi kama Bundesliga , baina ya Bayern Munich na Hamburg SV, katika pambano linalojulikana kama klasika ya kaskazini na kusini nchini Ujerumani. Bayern Munich ilishinda kwa mabao 8-0.

Fußball Bundesliga 21. Spieltag FC Bayern vs. Hamburger SV
Mlinda mlango wa Hamburg Jaroslav Drobny akiwa hana la kufanya baada ya bao kutinga wavuniPicha: Alexander Hassenstein/Bongarts/Getty Images

Mshambuliaji ambaye alikuwa akikosolewa wiki mbili zilizopita kwa kushindwa kufurukuta uwanja Mario Götze alipachika mabao mawili katika mchezo huo na amesema.

"Nafikiri tumeona kwamba tunaweza uwezo wa kucheza kandanda kwa raha. Lakini ni rahisi ukiwa mbele kwa mabao 3, na hapo ndio inakuwa rahisi zaidi. Tumeweza kucheza kwa urahisi kabisa. Tunatambua , kwamba Jumanne tunaanza tena mwanzo na ndio ilivyo kila wakati. Ilikuwa hivyo dhidi ya Stuttgart, na ndio ilivyokuwa leo na inatulazimu kujaribu kuendeleza hali hii, ambayo tumeionesha hii leo."

Kocha wa Hamburg SV Josef Zinnbauer alikuwa na maneno haya ya kujiliwaza.

"Nafikiri kipigo cha mabao 8 kwa bila hakiwezi kufanyiwa uchambuzi, kila mmoja anafahamu kile kilichokwenda kombo leo. Na tunapaswa kuwekwa sisi wote katika boti moja. Kwa muda wa wiki mbili tumecheza michezo miwili , ambayo tumeshinda na kupata pointi sita. Leo tumeshindwa , na kwa mabao 8 kwa bila kwa kweli ni maafa, na kwamba kwa kila shabiki na mhusika katika klabu hii ni kitu kinachotuonesha vibaya na siku mbaya kabisa kwetu."

Ilikuwa siku mbaya kabisa kwa Hamburg SV, lakini ilikuwa siku ya kufurahisha kwa mashabiki wa kandanda waliokuwa wakiangalia pambano kati ya Bayer Leverkusen na Wolfsburg. Wapenzi wa kandanda waliona mabao 9 yakikwama wavuni, lakini si kwa upande mmoja. Ulikuwa mchezo wa kuvutia kabisa ambapo Wolfsburg wakiwa wageni wa Leverkusen walitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 5-4. Alikuwa mshambuliaji wa Wolfsburg Bas Dost ambaye alikuwa kinara wa mabao siku hiyo akipachika mabao 4 wavuni. Si peke yake lakini mshambuliaji wa Bayer Leverkusen pia Heung-Min Son nae alipachika mabao 3.

Fußball Bundesliga 21. Spieltag Bayer 04 Leverkusen vs. VfL Wolfsburg Bas Dost
Shujaa wa Wolfsburg , Bas DostPicha: Dennis Grombkowski/Bongarts/Getty Images

Alipoulizwa Bas Dost iwapo hajawahi kufunga mabao mengi kama hayo katika mchezo mmoja alijibu.

"Hapana niliwahi mara kadhaa kufunga mabao mengi. Lakini mchezo wa leo ulikuwa wa aina yake, wa aina yake kabisa. Na vipi tuliweza kuongoza kwa mabao 3 kwa bila kwa kweli huwezi kuamini. Tulicheza vizuri sana katika nusu ya kwanza . Lakini mwishoni , kwa kweli ndio ilikuwa hivyo. Na hii inathibitisha uwezo wetu , kwamba hatukukata tamaa. Kipindi cha pili kilikuwa kibaya kwetu. Lakini pamoja na hayo tuliweza kushinda mchezo huu. Na kushinda ugenini nyumbani kwa Leverkusen kwa mabao 5-4 ni safi sana."

Fußball Bundesliga 21. Spieltag Bayer 04 Leverkusen vs. VfL Wolfsburg
Mpambano kati ya Bayer Leverkusen dhidi ya WolfsburgPicha: Dennis Grombkowski/Bongarts/Getty Images

Kocha wa Leverkusen Roger Schmidt ameueleza mchezo huo kuwa haukuwa wa kawaida.

"Mchezo huu umekwenda katika hali ya kustaajabisha kabisa. Nafikiri, tulipata nafasi ya kwanza nzuri lakini Wolfsburg walipata nafasi moja ya kwanza na wakaitumia kupata bao la kuongoza. Na pia katika mpira uliopigwa mita 70 uliweza kuingia wavuni. Na kuanzia hapo timu yangu ilijisikia hali ya kutojiamini kabisa. Walipoteza mwelekeo kabisa . Sio tu umiliki wa mpira lakini pia kupambana kuupata mpira na wakati huo Wolfsburg walikuwa juu na kufanya kila kitu kirahisi."

Fußball Bundesliga Borussia Dortmund vs. 1. FSV Mainz 05
Borussia Dortmund wakifurahia bao katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mainz 05Picha: Bongarts/Getty Images/L. Baron

Borussia Dortmund

Borussia Dortmund iliondoka kwa mara ya kwanza mwaka huu kutoka katika eneo la mkiani mwa ligi , baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mainz 05 siku ya Ijumaa na Werder Bremen iliendeleza hali ya kushangaza ya kufufuka kwa kuishinda Hoffenheim kwa mabao 3-2.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman