1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiswahili chawavutia wengi kusini DRC

Mohammed Khelef19 Juni 2015

Kiswahili ni lugha iliyotapakaa kote mashariki na kati ya Afrika ikiwa na chimbuko lake katika pwani ya Afrika Mashariki na sasa ndio lugha inayozungumzwa na sehemu kubwa ya wakaazi wa eneo hilo.

https://p.dw.com/p/1FjlQ
Mwalimu George Mulumbwa wa Chuo Kikuu cha Lubumbashi.
Mwalimu George Mulumbwa wa Chuo Kikuu cha Lubumbashi.Picha: Mohammed Khelef

[No title]

Unaposikia "Batu bawili bana biti bitatu" unafahamu nini? Watu wa kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekuwa wakitumia Kiswahili kwa karne kadhaa sasa, ila suali kubwa ni ikiwa wanatumia Kiswahili cha aina gani? Mhadhiri wa Kiswahili kwenye Chuo Kikuu cha Lubumbashi, George Mulumbwa, anazungumza na Mohammed Khelef kwenye Kiswahili Kina Wenyewe juu ya kukua na kutumika kwa Kiswahili kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.