1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

'WildLeaks' kufichua majingili wakubwa

2 Septemba 2014

Ujangili wa kuuwa Tembo na Vifaru barani Afrika kwa kiasi kikubwa umegubikwa na vyombo vya usalama vikishirikiana na mtandao wenye nguvu zaidi.

https://p.dw.com/p/1D5Nm
Bildergalerie Wilderei
Picha: STRINGER/AFP/Getty Images

Lakini makundi ya watetezi wa mazingira yamekua yenye kutoa taarifa kwa lengo la kuzuia vitendo hivyo.

Hii ni taarifa ya kwanza ya mtandao wa Wildleaks mtandao wenye kufanya kazi zake za utaoji taarifa kama ilivyo kwa ule mwengine maarufu duniani wa Wiki Leaks umejikita hasa katika saula la mazinguira na uhalifu wake. Wakati wawindaji haramu wakiwa katika makabiliano makali ya mtutu wa bunduki katika hifadhi mbalimbali za taifa za wanyama, majangili wakiendelea na mauwaji yao dhidi ya wanyama, mtandao huu sasa unaonekana kuwalenga wafanyabiashara hiyo ambayo wanajitengenezea kiasi kikubwa cha fedha.

Mwasisi wa mtandao huo, Andrea Costa, mshauri wa zamani katika masuala ya usalama na mwanamazingira wa muda mrefu alisimama na hapa namnukuu" Kwa mfano tumepata, mfano wa mtu mmoja nchini Kenya, mwenye muunganiko na serikali ya Kenya, ambae anashiriki katika biashara hiyo ya pembe za Ndovu".

Jitihada za kukusanya taarifa zinaendelea

Akizungumza bwana huyo kwa haraka haraka kwa kiingereza chenye lafudhi ya Kiitaliani alisema, mtu huyo sio rahisi kumuondoa katika mtandao. Wana nguvu kubwa, na kufanya hivyo utahitaji nguvu nyingine ya ziada kutoka nje. Hata hivyo aliongeza kusema kwa hivi sawa wapo katika jitihada za kukusanya taarifa zaidi.

Bildergalerie Wilderei
Uteketezaji wa pembe za Ndovu mjini GabonPicha: picture-alliance/James Morgan/WWF

Kasi ya vitendo vya ujangili vimeongezeka katika maeneo mengi barani Afrika, vikichochewa na mahitaji ya Pembe za Ndovu na Vifaru huko barani Asia, ambavyo vimekuwa vikitumika kama dawa za asili na viashiria vya kuonyesha hadhi kwa wakazi wengi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu,jijini Dar es Salaam, Tanzania Costa alipigia kifua imani yake kuwa kutumika kwa jukwaa la katika mtandao kunaweza kuwa sehemu ya vita dhidi ya vitendo vya ujangili. Ukiwa umezinduliwa Februari mwaka huu WildLeaks uliweza kupata taarifa ya kwanza katika kipindi kisichozidi masaa 24.

Jitihada za mtandao huo wa WildLeaks

Tangu wakati huo mtandao umeweza kupata taarifa 45, ambapo 28 miongoni mwa hizo zimeonekana kuwa na umuhimu. Taarifa zenyewe zimehusisha shida mbalimbali za kimazingira duniani ikiwemo uwindaji haramu wa mnyama Chui huko Sumatra, biashara haramu ya magogo Urusi na Mexico, na uuzwaji haramu wa bidha zitokanazo na wanyama nchini Marekani.

Mtandao wa WildLeaks, umeweza kutoa taarifa vyombo vya dola kwa baadhi ya mataifa huku nyingine wakibadilishana na taasisi nyingine za utunzaji mazingira katika maeneo husika. Baadhi ya taarifa hizo zipo katika uchunguzi wa mtandao huo. Matukio mawili ya uchunguzi wa kina yameanza, wakati mengine mawili yanatarajiwa kuanza Septemba.

Aidha mtandao huo umeacha jukwaa wazi kwa wenye taarifa za siri bila kutaja majina yao kwa lengo la kuwalinda kiusalama. Hatua hii inatajwa kuwa ni namna mpya ya kukabiliana na ujangili na kwamba wadau katika sekta ya uhifadhi wa mazingira wameipokea kwa mikono miwili.

Richard Thomas kutoka katika taasisi moja inayojihusisha na uchunguzi wa uhalifu wa wanyamapori alisema alisema hiyo ni hatua mpya katika katika kukabiliana na uhalifu. Lakini Costa, akiwa Dar es Salaam, ambae anaratibu mtandao huo alisema changamoto kubwa, kunahitajika watu wautambue na kuwepo na imani kwa watu wanaojihusisha nao.

Theluthi moja ya pembe haramu za ndovu ambazo zimekamatwa bara la Asia zinaelezwa kutoka Tanzania.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP
Mhariri: Josephat Charo